Friday, 27 April 2012

ROMA MKATOLIKI KUYAWEKA MAISHA YAKE YA MZIKI KWENYE DOCUMENTARY YAKE MPYA.

Msanii anayeiwakilisha TANGA katika bongo fleva ROMA, baada ya kuchukua tuzo mbili za Kilimanjaro kama Msanii bora wa Hip Hop na wimbo wake Mathematics kuchukua kama wimbo bora wa Hip Hip hivi sasa anatengeneza Documentary yake inayoeleza maisha yake kimuziki toka alivyoanza mziki shida alizopitia mpaka kufikia hivi sasa alipofikia.
  
    Roma akiwa katika studio ya Tongwe Rec akiitengeneza DVD hiyo ambayo amesema nimapema sana kusema itatoka lini ila haitochelewa kutoka na anaamini watu wataipenda na italeta utofauti kidogo maana story iliyomo ndani ya Documentary hiyo iko kitofauti na itamgusa kila mmoja.

No comments:

Post a Comment